TAMWA, PEGAO NA ZAFELA ZAFANYA ZIARA VIJIJINI KUANGALIA MAFANIKIO NA CHANGAMOTO ZA WANANCHI-MRADI WA SWIL.
IMEANDIKWA NA HASSAN MSELLEM, PEMBA.
Katika kutamatisha uketelezaji wa
mradi wa Uhamasishaji wa Wanawake katika Uongozi (SWIL) chama cha waandishi wa
habari wanawake Tanzania ‘TAMWA’ Jumuiya Utetezi wa Mazingira na Kijinsia Pemba
‘PEGAO’ na Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar ‘ZAFELA’ zimefanya ziara
maalumu ya kuangalia mafanikio na kusikiliza changamoto katika Skuli ya Msingi
Kunguni na Familia yenye watoto watano wenye ulemavu wa viungo katika kijiji
cha Kwa-Azani Wambaa ili kuweza kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo.
Rashid Omar Ali, ni mwalimu Mkuu wa
Skuli ya Msingi Kunguni amesema kupitia mradi wa SWIL wamefanikiwa kuongeza idadi
ya vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo pamoja na walimu, mafanikio ambayo
yamechangia kwa kiasi kikubwa kuongeza idadi ya ufaulu kwa wanafunzi wa darasa
la saba kutoka wanafunzi wawili mwaka 2022 hadi wanafunzi saba mwaka 2023.
Aidha amesema licha mafanikio hayo bado wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji na kuziomba taasisi hizo kuzungumza na mamlaka husika ili kuipatia ufumbuzi changamoto hiyo.
“Kwakweli mradi wa SWIL umetusaidia sana maana tukuiwa tuna changamoto
nyingi sana ikiwemo uhaba wa madarasa matundu ya vyoo walimu na maji lakini
kwasasa tumeongeza madarasa sana walimu saba na matundu ya vyoo tunashukuru si
haba na ukiangalia hata idadi ya ufaulu wa wanafunzi umeongeza mwaka huu kwani
tumepasisha wanafunzi saba na ikiwemo kipawa mmoja sasa hivi changamoto
inayotukabili maji tu” alisema mwalimu mkuu huyo
Kwa upande wake mumahamishaji jamii Wilaya ya Mkoani Kassim Nassor Iddi, amesema mafanikio hayo yametokana na mikutano ya kijamii na kamati ya Skuli hiyo ambapo wananchi walieleza changamoto zinazoikabili Skuli hiyo na hatimae kuzifanyia kazi changamoto hizo.
Wakati huo huo Viongozi wa mradi huo wa SWIL waliitembelea familia yenye watoto sita wenye ulemavu wa miguu kwenye kijiji cha Kwa-Azani Wambaa ili kufahamu changamoto zinazoikabili familia hiyo nakuzipatia ufumbuzi kwa kushirikiana na wadau mbali mbali.
Fatma Simai Faki, ni mama mzazi wa
watoto sita wenye ulemavu wa viungo amesema tatizo hilo la ulemavu wa miguu kwa
watoto hujitokeza katika kipindi cha ukuaji hali inayopelekea kushindwa
kutembea kwa watoto hao.
Alisema “Tatizo hili ulemavu wa miguu hawakuzaliwa nalo bali hujitokeza katika
kipindi chao cha ukuwaji wakiwa na umri kuanzia miaka kumi na kuendelea huanza
kutembea kwa shida sana kwani miguu yao huwa mizito sana wanashindwa kupiga
hatua vizuri hutembea kwa kujiburuta na kuanguka anguka na kisha kushindwa moja
kwa moja kutembea”
Alieleza changamoto zinazowakabili ni
pamoja na kutokutambuliwa na jumuiya yoyote ya watu wenye ulemavu hali
inayopelekea kukosa misaada mbali mbali ikiwemo matibabu ingawa amesema tayari
wamepatiwa msaada wa viti mwendo viwili ambavyo alisema vinashindwa kukidhi
mahitaji ya watoto hao kutokana umri wao na udhaifu wa viti mwendo hivyo.
“Tangu watoto wangu wapate matatizo haya sijaona taasisi yoyote wala kiongozi yeyote ambaye amekuja kutupatia msaada Fulani labda hivi karibu ndio ulikuja uongozi wa baraza la watu wenye ulemavu Wilaya ya Mkoani kupitia ufadhili wa wametupatia viti mwendo viwili navyo vimeshindwa kuwasaidia kwasababu hawa watoto ni wakubwa sasa kwa hivyo maringi ya hivi viti yanapinda hali inayopelekea viti hivyo kutokukidhi haya” alisema
Mkurugenzi wa PEGAO Hafidh Said Abdi,
amesema katika utekelezaji wa mradi huo wa miaka minne wenye shebaha ya
kuwafikia wananchi 6,000 Unguja na Pemba, wamefanikiwa kufakia wananchi 6,895
ambapo miongoni mwa wananchi hao wanwake ni 4,568 na wanaume ni 2,327 idadi
ambayo tayari imefikiwa kwa upande wa kisiwa cha Pemba pekee.
Na kwa upande wa uhamasishaji jamii kupitia vyombo vya habari Mratibu wa Tamwa Kisiwani Pemba Bi. Fat-hiya Mussa Said, amesema jumla ya wananchi 2,194 ambapo miongoni mwa wananchi hao wanawake ni 1,222 na wanaume ni 972 pamoja na kuwajengea uwezo wandishi wa habari 166 ambao wameweza kuadika habari na malaka mbali mbali za takwimu za wanawake na uongozi zinazofikia 1,588.
Akizungumza kwa nyakati tofauti
katika ziara hiyo Mratibu wa mradi wa ‘SWIL’ Bi. Mariam Ame, amesema kupitia
mradi wa SWIL wamefanikiwa kuchangia katika utatuzi wa changamoto mbali mbali
za kijamii ikiwemo kuwapatia vitambulisho vya Mzanzibari mkaazi kwa wananchi,
vyeti vya kuzaliwa, ujenzi wa vituo vya mama na mtoto, ujenzi madarasa, kutoa
misaada kwa watu wenye ulemavu na hali ngumu zakimaisha pamoja kuwahamasisha
akina mama kujiunga na vyama vya sisasa ili waweze kupata nafasi ya kushiriki
katika nafasi mbali mbali za uongozi kupitia vyama vyao vya siasa na Serikali
kwa ujumla.
Ziara hiyo yenye lengo la kuangalia
mafanikio na changamoto kupitia mradi wa ‘SWIL’ imewajumuisha viongozi wa Chama
cha Wandishi wa Habari Wanawake Tanzania ‘Tamwa’ kanda ya Pemba, viongozi wa
Jumuiya ya Utetezi wa Kimazingira na Kijinsia Pemba ‘PEGAO” pamoja na watendaji
wa Jumuiya ya wanasheria wanawake Zanzibar ‘ZAFELA’.














Comments
Post a Comment