JUMUIYA YA ‘PEPOHUDA’ YATOA MAFUNZO KWA WASICHANA NA MSAADA WA TAULO ZA KIKE.
Imeandikwa Na, Hassan Msellem.
Wanafunzi Kisiwani Pemba wametakiwa kujiepusha na vitendo viovu ikiwemo mahusiano ya kimapenzi ili kuepukana na madhara yanayoweza kujitokeza.
Kauli hiyo imetolewa na
Mwenyekiti Baraza la Mji Wete Bi. Zulfa Abdalla Saidi, wakati akifunga mafunzo
ya afya ya uzazi kwa wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Chasasa yaliyotolewa na
Jumuiya kupunguza umaskini na kuboresha maisha ya watu Pemba (PEPOHUDA) huko
Jadida Wete, amesema kumekuwepo kwa taarifa za wanafunzi wanaojihusisha na
mahusiano ya kimapenzi hali inayopelekea kufanya vibaya katika masomo yao
pamoja na kushindwa kuendelea na masomo.
Kwa upande wake mwakilishi
kutoka Ofisi ya Mrajis wa jumuiya zisizo za Kiserikali Kisiwani Pemba Bi. Sada
Abuubakar Khamis, amesema kutolewa kwa mafunzo hayo afya ya uzazi kwa wanafunzi
hao kutawasaidia kukabiliana na changamoto mbali mbali ikiwemo kujikinga na
mimba za umri mdogo.
Mratibu wa Jumuiya ya
Pepohuda Said Mbarouk Juma, alisema utolewaji wa mafunzo hayo ni mwendelezo wa
utekelezaji wa mradi wa kuongeza uelewa wa haki za afya ua uzazi kwa watoto na
vijana wa kike ili kuwakinga na mimba za umri mdogo.
Mratibu wa Jumuiya ya PEPOHUDA Said Mbarouk Juma.
Akiwasilisha mada ya
Mawasiliano na Madhara ya Mimba za umri mdogo Bi. Hudhaifa Said Salum, amesema
miongoni mwa madhara yanayoweza kujitokeza katika mimba za umri mdogo ni pamoja
na kukatisha masomo, kupoteza damu nyingi kipindi cha kujifungua pamoja vifo.
Katika kukabilaiana na
vitendo vya udhalilishaji Mkufunzi wa mafunzo hayo Mwanaisha Amani Salum,
aliwataka wasichana hao kutoa taarifa pindi wanapofanyiwa vitendo hivyo pamoja
na kujiepusha na marafiki waovu.
Sheha wa Shehia ya Mtemani
Mrisho Juma Mtumwa, aliwasihi wanafunzi hao kuyafanyia kazi mafunzo hayo ili
yaweze kuwasaidia masomo yao.
Nao wanafunzi hao wameishukuru jumuiya ya PEPOHUDA kwa kuwapatia mafunzo hayo na kuahidi kuyafanyia kazi ili lengo la utolewaji wa mafunzi hayo liweze kufikiwa.
Mafunzo hayo ya siku moja
yametoelewa na jumuiya kupunguza umasikini na kuboresha maisha ya watu Pemba ‘PEPOHUDA’
kwa ufadhili wa Shirika la Y+ Global kupitia mfuko wa Her Voice Fund.


















Comments
Post a Comment