Posts

Showing posts from March, 2024

"Kumalizika kwa mradi wa SWIL isiwe sababu ya kubweteka kuzifanyia kazi changamoto za kijamii-CB" DC Chake Chake.

Image
Imeandikwa na Hassan Msellem, Pemba. Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Ndugu Abdalla Rashid Ali, amewataka Wahamasishaji Jamii (CB) Kisiwani Pemba ambao walikuwa wadau wakubwa katika utekelezaji wa Mradi wa uhamasishaji Wanawake katika Uongozi (SWIL) kuendelea kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili Wananchi ili ziweze kupatiwa ufumbuzi. Mkuu huyo wa Wilaya ametoa kauli hiyo huko katika ukumbi wa Maktaba Chake Chake wakati alipokuwa akifunga huo wa miaka minne, amesema kumalizika kwa mradi huo kumeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa katika utatuzi wa changamoto mbali mbali za Kijamii na Uongozi kwa Wanawake. Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Ndg. Abdalla Rashid Ali. Mratibu wa Jumuiya ya Utetezi wa kijinsi na mazingira Pemba (PEGAO) Bi. Dina Juma Makota amesema kupitia mradi huo wamefanikiwa kuwafikia Wananchi 6,894 idadi ambayo imepindua shebaha ya mradi huo kwa upande wa Kisiwa cha Unguja na Pemba ambayo ni kuwafikia Wananchi 6000 kwa kipindi cha miaka 4 ya utekelezaji wake. Mratibu wa PEGAO B...