Posts

"Kumalizika kwa mradi wa SWIL isiwe sababu ya kubweteka kuzifanyia kazi changamoto za kijamii-CB" DC Chake Chake.

Image
Imeandikwa na Hassan Msellem, Pemba. Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Ndugu Abdalla Rashid Ali, amewataka Wahamasishaji Jamii (CB) Kisiwani Pemba ambao walikuwa wadau wakubwa katika utekelezaji wa Mradi wa uhamasishaji Wanawake katika Uongozi (SWIL) kuendelea kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili Wananchi ili ziweze kupatiwa ufumbuzi. Mkuu huyo wa Wilaya ametoa kauli hiyo huko katika ukumbi wa Maktaba Chake Chake wakati alipokuwa akifunga huo wa miaka minne, amesema kumalizika kwa mradi huo kumeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa katika utatuzi wa changamoto mbali mbali za Kijamii na Uongozi kwa Wanawake. Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Ndg. Abdalla Rashid Ali. Mratibu wa Jumuiya ya Utetezi wa kijinsi na mazingira Pemba (PEGAO) Bi. Dina Juma Makota amesema kupitia mradi huo wamefanikiwa kuwafikia Wananchi 6,894 idadi ambayo imepindua shebaha ya mradi huo kwa upande wa Kisiwa cha Unguja na Pemba ambayo ni kuwafikia Wananchi 6000 kwa kipindi cha miaka 4 ya utekelezaji wake. Mratibu wa PEGAO B...

TAMWA, PEGAO NA ZAFELA ZAFANYA ZIARA VIJIJINI KUANGALIA MAFANIKIO NA CHANGAMOTO ZA WANANCHI-MRADI WA SWIL.

Image
IMEANDIKWA NA HASSAN MSELLEM, PEMBA.   Katika kutamatisha uketelezaji wa mradi wa Uhamasishaji wa Wanawake katika Uongozi (SWIL) chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania ‘TAMWA’ Jumuiya Utetezi wa Mazingira na Kijinsia Pemba ‘PEGAO’ na Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar ‘ZAFELA’ zimefanya ziara maalumu ya kuangalia mafanikio na kusikiliza changamoto katika Skuli ya Msingi Kunguni na Familia yenye watoto watano wenye ulemavu wa viungo katika kijiji cha Kwa-Azani Wambaa ili kuweza kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo.   Rashid Omar Ali, ni mwalimu Mkuu wa Skuli ya Msingi Kunguni amesema kupitia mradi wa SWIL wamefanikiwa kuongeza idadi ya vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo pamoja na walimu, mafanikio ambayo yamechangia kwa kiasi kikubwa kuongeza idadi ya ufaulu kwa wanafunzi wa darasa la saba kutoka wanafunzi wawili mwaka 2022 hadi wanafunzi saba mwaka 2023.   Aidha amesema licha mafanikio hayo bado wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji na kuz...

JUMUIYA YA ‘PEPOHUDA’ YATOA MAFUNZO KWA WASICHANA NA MSAADA WA TAULO ZA KIKE.

Image
 Imeandikwa Na, Hassan Msellem. Mwenyekiti Baraza la Mji Wete Bi. Zulfa Abdalla Saidi, akikabidhi taulo za kike kwa mwanafunzi. Wanafunzi Kisiwani Pemba wametakiwa kujiepusha na vitendo viovu ikiwemo mahusiano ya kimapenzi ili kuepukana na madhara yanayoweza kujitokeza. Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti Baraza la Mji Wete Bi. Zulfa Abdalla Saidi, wakati akifunga mafunzo ya afya ya uzazi kwa wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Chasasa yaliyotolewa na Jumuiya kupunguza umaskini na kuboresha maisha ya watu Pemba (PEPOHUDA) huko Jadida Wete, amesema kumekuwepo kwa taarifa za wanafunzi wanaojihusisha na mahusiano ya kimapenzi hali inayopelekea kufanya vibaya katika masomo yao pamoja na kushindwa kuendelea na masomo. Kwa upande wake mwakilishi kutoka Ofisi ya Mrajis wa jumuiya zisizo za Kiserikali Kisiwani Pemba Bi. Sada Abuubakar Khamis, amesema kutolewa kwa mafunzo hayo afya ya uzazi kwa wanafunzi hao kutawasaidia kukabiliana na changamoto mbali mbali ikiwemo kujikinga na mimba za ...